Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inonga amwagiwa sifa kila kona

Henock Inonga Baka Kazi Mlinzi wa Simba, Henock Inonga Baka amepata nafasi ya kuingia kwenye kikosi cha CAF

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kitendo cha beki wa Simba, Henock Inonga kuwa katika kikosi cha wiki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kimewafanya wachezaji wakongwe wamwagie sifa kwa kupenya kwake mbele ya mastaa mbalimbali Afrika.

Kikosi hicho kimetolewa baada ya timu zote kucheza mechi ya tatu kwenye makundi ndipo Inonga akawamchezaji pekee ambaye amechaguliwa katika kikosi cha wiki Ligi ya Mabingwa kutoka timu ya Simba.

Mshambuliaji wa zamani Simba, Bakari Kigodeko alisema kitendo cha mchezaji huyo kuwepo katika kikosi cha wiki kwenye Ligi ya Mabingwa inatokana na kujituma kwake.

"Ni beki mzuri na anajituma na ndio maana anapokosekana kwenye timu kuna kitu kinapungua ndani ya Simba, ukizungumzia upande wa mabeki wa kati wanaofanya vizuri huwezi kumuacha yeye," alisema Kigodeko.

Wakati huo huo mchezaji wa zamani Simba na Yanga, Zamoyoni Mogela alisema hashangazwi na kuona beki huyo yupo kwenye kikosi cha wiki cha Ligi ya Mabingwa kwa sababu anajituma sana.

"Mpira ni mchezo wa wazi na hadi watu wamekaa na kumchagua maana yake wameona kitu kutoka kwake, anaisaidia Simba na ndio maana kule Uganda aliifungia bao timu yake wakati washambuliaji wameshindwa," alisema Mogela.

Wachezaji wengine waliopo kwenye kikosi ni kipa Farid Ouedraogo (As Vita), Mustafa Karshoum (Al Merreikh), Jamal Harkass (Wydad Casabalanca), Raed Bouchniba (Esperance), Lema Chikito (As Vita) na Mohamed Ben Romdhane (Esperance).

Simba yenye pointi tatu inatarajia kucheza mchezo wake wa nne dhidi ya Vipers, Machi 7 saa 1:00 usiku katika uwanja wa Mkapa.

Wengine ni Hussein El Shahat (Al Ahly), Paulo Sergio (Al Merreikh), Makabi Lilepo (Al Hilal) na Peter Shalulile (Mamelod Sundowns).

Chanzo: Mwanaspoti