Henock Inonga mlinzi wa kati wa timu ya Taifa ya Congo DR na Klabu ya Simba hapo jana Usiku hakuthubutu kuangalia penalty hata moja wakati kipa wa Bafana Bafana, Ronwen Williams akiharibu sherehe ya Congo DR kutwaa Bronze Medals.
Inonga hakutaka kuona tukio hili aliamua kuangalia upande mwingine hadi penati ya mwisho iliyopigwa na Meshack Elia ikatua katika mikono ya Williams na kuipa ushindi Afrika Kusini kwa penati 6-5.
Ni wazi kwamba, Inonga ni mwoga sana unapokuja wasaa wa kupigiana penati tano tano licha ya ubora wake ndani ya pitch lakini inaonesha havutiwi kabisa kipengere hiki cha mikwaju ya penati.
Inonga aliwahi kuichoma Simba nchini Afrika Kusini kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCL) hatua ya robo fainali dhidi ya Orlando Pirates kwa kukosa penati na Simba kuondoshwa kwenye michuano hiyo.
Kumbuka kuwa, hata Kocha wa Liverpool ya Uingereza, Jurgen Klop huwa hapendi kushuhudia mikwaju ya penati ikipigwa timu yake ikifika kwenye hatua hizi.