Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inonga acheza mechi ya kwanza ya Kimashindano na DR Congo

Inonga Congo Mlinzi wa Simba na Timu ya DR Congo, Henock Inonga

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Simba, Enock Inonga usiku wa jana ameanza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha DR Congo kwenye mechi ya kimashindano tangu timu hiyo ilipoanza kunolewa na Mfaransa, Sebastien Desabre.

Mchezaji huyo ni miongoni mwa nyota 11 ambao kocha Desabre amechagua kuanza nao dhidi ya Mauritania katika mchezo huo ambao DR Congo ipo nyumbani wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia.

Katika kikosi cha jana, Inonga atacheza nafasi ya beki wa kati sambamba na nahodha Mbemba Chancel.

Kikosi cha DR Congo kinachoikabili Mauritania usiku wa jana kilikuwa na nyota kama na Lionel Mpassi, Gedeon Kalulu, Inonga, Mbemba, Joris Kayembe, Charles Pickel, Meschack Elia, Samuel Moutossamy, Bakambu Cedric, Gael Kakuta na Yoan Wissa.

Marefa wa mechi hiyo walitoka Libya ambao ni Elmabrouk Muhammad, Mohammed Faraj, Alayat Munji na Mohamed Agha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live