Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inonga: Njooni Uwanjani tumalize kazi

Inonga BAKA Henock Inonga

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki kipenzi cha mashabiki wa Simba kwasa, Henock Inonga ambaye alihusika kwa kufunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga, amewaambia mashabiki waende kwa wingi uwanja Jumamosi wao watafanya kazi yao.

Inonga ambaye kabla ya kutua Simba, alikuwa akihusishwa na Yanga, alisema dhidi ya watani yameongeza morali kwao na wataendeleza ubora wao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca kwenye uwanja wa Mkapa.

"Tumetoka kucheza mechi kubwa na timu ambayo inaongoza msimamo wa ligi na tumepata matokeo ni kipimo chetu sahihi kuelekea mchezo wa Jumapili tunaendelea kujifua na kujiweka imara kwaajili ya mchezo huo ambao pia ni muhimu kwetu;

"Wydad ni timu nzuri tutaingia kwa kuwaheshimu kwani na sisi pia tuna kikosi kizuri ambacho kipo kwenye hali nzuri ya ushindani dakika 90 za zitaamua ubora wa timu zote mbili lakini kwa upande wetu tunapambana kuhakikisha tunatumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani,"alisema Inonga huku akiwaomba mashabiki waje kwa wingi kuwaongezea mzuka.

Pia amefichua siri ya ubora wa Ally Salim kwenye mchezo wa Yanga, kuwa ni namna benchi la ufundi lilimuandaa huku akikiri kuwa alikuwa na kazi maalum kuhakikisha anamfanya anakuwa makini langoni ili waweze kutoka bila kuruhusu bao.

"Ni moja ya mchezo bora uliochezwa kwa kuzikutanisha Simba na Yanga kwenye mchezo huo mbali na jukumu lanhu la kuhakikisha nazuia mashambulizi langoni kwetu pia nilikuwa na jukumu la kumjengea kujiamini Salimu kwasababu ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza wa dabi;

"Nilimwambia ni mchezo mkubwa kwako unatakiwa kuwa imara langoni timu yote ya Simba ipo pamoja na yeye anatakiwa kufanya kwa ukubwa na ubora ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kujiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kuaminiwa," alisema Inonga ambaye ni raia wa DR Congo.

Inonga alisema alimwambia Salimu kuwa kuaminiwa kwake kwa kupewa mechi kubwa unaweza ukawa mwanzo mzuri kwake kwenye majukumu yake huku akimtaka kutumia nafasi hiyo kuzungumza na walinziwake waweze kumbeba kwa kumpunguzia majukumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live