Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inonga, Mayele uhakika AFCON 2023

Mayele X Inonga Inonga, Mayele uhakika AFCON 2023

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki kisiki wa Simba, Henock Inonga na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele anayekipiga Pyramid FC ya Misri, wamepenya kwenye kikosi cha mwisho wachezaji 24 wa timu ya taifa ya DR Congo kitakachoiwakilisha nchi hiyo kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023, zitakazofanyika Ivory Coast.

DR Congo ipo kundi F na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Morocco na Zambia na fainali hizo zitaanza Januari 13 hadi Februari 14, 2024.

Makipa: Dimitry Bertaud, Siada Baggio na Lionel Mpasi

Mabeki: Inonga Baka, Rock Bushiri, Gédeon Kalulu, Chancel Mbemba, Dylan Batubinsika na Arthur Masuaku, Kayembe na Brian Bayeye.

Viungo: Meshack Elia, Théo Bongonda, Edo Kayembe, Gael Kakuta, Charles Pickel, Samuel Moutoussamy, Aaron Tshibola, Silas Katompa na Grady Diangana.

Washambuliaji: Fiston Mayele, Cedric Bakambu, Yoane Wissa na Simon Banza

Chanzo: www.tanzaniaweb.live