Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inonga, Mayele historia imeandikwa kwenye vitabu vya soka

Inonga Hakimi.jpeg Inonga, Mayele historia imeandikwa kwenye vitabu vya soka

Sun, 11 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya DR Congo kufungwa kwa penalti 6-5 dhidi ya Afrika Kusini katika mechi ya kuwania mshindi wa tatu wa michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023, nyota wa Simba, Henock Inonga, ameingia katika vitabu vya kumbukumbu.

Inonga na nyota wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele ambaye sasa anaitumikia klabu ya Pyramids FC ya Misri, wote wanaingia katika historia tamu ya taifa la Congo walioipigania vyema nchi yao kwenye Afcon.

Mastaa hao wameiwezesha DR Congo kumaliza katika nafasi ya nne ya michuano hiyo kwa mara ya pili 2023 baada ya taifa hilo kumaliza katika nafasi hiyo pia katika fainali za 1972.

Hii pia ni mara ya sita kwa taifa hilo kumaliza ndani ya Top 4 ya michuano hiyo ililibeba taji hilo mara 2 (1968, 1974) na kisha ikamaliza katika nafasi ya tatu mara mbili pia (1998, 2015). Kiufupi, DR Congo haijawahi kumaliza katika nafasi ya pili, ikimaanisha ilipofika fainali ilibeba mara zote mbili.

Wapinzani wao, Bafana Bafana ya Afrika Kusini kwa kuifunga DR Congo jana wameshika nafasi ya 2 kwa mara ya pili (2000, 2023).

Hii ni mara ya nne kwa Bafana Bafana kumaliza ndani ya Top 4, kwani imelitwaa taji hilo mara moja mwaka 1996 na katika fainali zilizofuata za 1998 ilishika nafasi ya pili. Yaani ikitinga nusu fainali haijawahi kushika nafasi ya nne.

Katika mechi ya jana usiku, Inonga hakuchezeshwa kabisa, baada ya kocha wao Sebastien Desabre kuamua kuwapa nafasi wachezaji ambao hawakupata kucheza mara kwa mara tangu mwanzo wa fainali hizi.

Katika mechi 7 za fainali hizi, Inonga amecheza mechi tano akiikosa moja tu ya makundi dhidi ya Tanzania ambayo alikuwa majeruhi iliyoisha kwa 0-0 na ya jana ya kuwania mshindi wa tatu.

Mayele alianzishwa katika mechi moja tu dhidi ya Tanzania katika hatua ya makundi huku nyingine akiingia kutokea benchini kama ilivyokuwa jana, ambako hakupewa kupiga penalti wakilala kwa penalti 6-5 baada ya dakika 120 kumalizika kwa matokeo ya 0-0.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live