Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Injinia Hersi unastahili maua yaliyochumwa Bustan ya Edeni

Hersi Mmss Injinia Hersi unastahili maua yaliyochumwa Bustan ya Edeni

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati unaichukua timu kutoka kwenye viganja vya mikono ya "Mshindo Msola." Sikuamini kama una miujiza ya kuifikisha Yanga nchi ya ahadi. Binafsi niliamini umekuja Jangwani kutafuta kick. Lengo uongeze idadi ya followers Instagram.

Nisamehe Engineer, ubongo wangu ulienda likizo ya kufikiri. Nilikuwa juu ya kilele cha upotofu wa fikra zangu zama zile.

Ulipokuwa ukienda Congo kuwafuata kina Fiston Mayele, Shabani Juma, Joyce Lomalisa na Bangala. Nilijua una mpango wa kuanzisha bendi itayompa challenge "Christian Bella."

Sikujua kama umefuata material ya kutengenezea silaha za maangamizi dhidi ya wekundu wa msimbazi. Leo umepora ufalme wa Simba. Zile goal 5 ni kishindo cha anguko la mnara wa babeli.

Mashabiki wa Yanga wakipewa tenda ya kuandika Biblia ya soka. Naamini jina "HERSI" litakuwa sehemu ya injili takatifu.

Unastahili maua yaliyochumwa bustani ya Eden injinia. Kama shukrani kwa kufanikiwa kuurudisha utukufu jangwani.

Kuitoa timu ghetto ilikokuwa ikijiendesha kwa nguvu ya bakuli. Hadi kucheza fainal ya Caf confederation. Kwa hili, unaidai mioyo ya mashabiki wa Yanga tattoo nzuri ya jina lako.

Hata zile goal 5 dhidi ya simba lupaso November 5. Yale ni matunda baada ya wewe kushinda vita ya kuigombea saini ya Azizi Ki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live