Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Infantino amlilia Issa Hayatou

Ayatou.png Infantino amlilia Issa Hayatou

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la Kimataifa ya Soka (FIFA), Gianni Infantino ametuma salamu za rambirambi kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa shirikiho hilo la Afrika, Issa Hayatou.

Hayatou alifariki dunia jana Alhamisi akiwa na umri wa miaka 77, huku akikumbukwa kama Rais aliyeiongoza CAF kwa miaka mingi zaidi 29, akichukua nafasi hiyo tangu mwaka 1988 hdi alipoondoka 2017.

Infantino ametuma salamu za rambirambi kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiandika: "Nimesikitishwa kupokea taarifa za kifo cha aliyekuwa Rais wa CAF, Makamu wa Rais wa FIFA na Mjumbe wa Baraza la FIFA, Issa Hayatou." Ulisomeka ujumbe wa Infantino na kuendelea; 

"Alikuwa shabiki wa michezo wa soka, alijitolea maisha yake kwa usimamizi wa michezo wa soka.

"Kwa niaba ya FIFA, rambirambi ziende kwa familia yake, marafiki, wafanyakazi wenzake wa zamani na wote wanaomfahamu. Pumzika kwa amani."

Agosti 2021 Hayatou alipigwa marufuku ya mwaka mmoja na FIFA kwa kukiuka kanuni za maadili wakati wa kusaini mkataba mkubwa zaidi kuwahi kutokea barani Afrika na kampuni ya habari ya Ufaransa ya Lagardere mnamo 2016.

Adhabu hiyo ilibatilishwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo mnamo Februari mwaka 2017.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live