Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Infantino alaani nyimbo za kibaguzi dhidi ya Lukaku

Lukaku Rumelu Lukaku

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa FIFA Gianni, Infantino amelaani kelele za ubaguzi wa rangi kutoka kwa mashabiki wa Juventus dhidi ya mshambuliaji wa Inter Romelu Lukaku wakati wa mechi yao ya nusu fainali ya kwanza ya Coppa Italia.

Lukaku alifunga mkwaju wa penalti dakika za lala salama na kuwafanya wageni Inter wapate sare ya 1-1 mjini Turin Jumanne, akisherehekea kwa kushika kidole mdomoni mbele ya wafuasi wa Juve kama jibu lao baada ya kumbagua.

Sherehe hiyo ilionekana kuwa ya uchochezi na Mbelgiji huyo alifukuzwa uwanjani kwa kosa la pili ambalo haliwezi kuzuilika, na tukio hilo lilisababisha makabiliano kati ya seti hizo mbili za wachezaji.

Lukaku alitoa taarifa hapo jana akitaka mamlaka ya Italia ichukuliwe hatua, ambayo imekuwa ikiungwa mkono na watu wengine wakubwa katika ulimwengu wa soka na Infantino alizitaja nyimbo hizo kuwa hazikubaliki na kutaka waliohusika waadhibiwe.

Infantino alisema: “Kandanda haina nafasi ya ubaguzi wa rangi au aina yoyote ya ubaguzi. Haikubaliki kuona unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi unaolengwa na watazamaji kwa mshambuliaji wa Inter Romelu Lukaku wakati wa mechi ya Coppa Italia huko Juventus huko Turin.”

FIFA na mimi tunasimama pamoja na Romelu Lukaku, kama tunavyofanya na mchezaji mwingine yeyote, kocha, afisa wa mechi, shabiki au mshiriki katika mechi ya soka ambaye amekumbwa na ubaguzi wa rangi au aina yoyote ya ubaguzi. Waathiriwa wa dhuluma hizo lazima waungwe mkono, na wahusika waadhibiwe na mamlaka zote.

Infantino amesema kuwa anarudia wito uliotolewa mwanzoni mwa mwaka huu kwa mashabiki kusimama na kuwanyamazisha wabuguzi hao. Alisema kuwa katika mpira wa miguu wanahitaji kuhakikisha kuwa vikwazo vikali vya michezo vinatumika kushugulikia matukio kama haya na kutumika kama kizuizi.

Katika ujumbe wa Lukaku mapema siku hiyo, alikuwa na hamu ya kuangazia jinsi matukio kama haya yanajirudia badala ya kutengwa.

Lukaku alisema kuwa; “Historia inajirudia. Nimeipitia mwaka wa 2019 na sasa 2023 tena. Natumai ligi itachukua hatua kweli wakati huu kwa sababu mchezo huu mzuri unapaswa kufurahishwa na kila mtu. Asante kwa jumbe za kuunga mkono kupinga ubaguzi wa rangi.”

Ujumbe wake umeungwa mkono na watu kama Kylian Mbappe ambaye aliandika kwenye Instagram: “2023 na bado matatizo yale yale. Lakini hatutakuacha ukabaliane nayo mwenyewe.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live