Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, amejibu ukosoaji unaotolewa kwa Qatar kuhusu madai ya ukiukwaji haki za Binadamu akisema huu ni unafiki wa Mataifa ya Magharibi.
Infantino ameyasema hayo jana siku moja tu kabla ya ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Dunia leo Jumapili.
Amesema kile kinachoendelea ni unafiki wa hali ya juu huku akisema kila mmoja anapaswa kuwa huru kumuunga mkono Mtu au kundi lolote analolitaka.
Amesema kile Ulaya ilichokifanya miaka 3000 iliyopita inapaswa iwe ikiomba msamaha kwa miaka mingine 3000 Ijayo kabla ya kuanza kutoa ushauri wa maadili kwa Watu ambapo amesema ukosoaji ni muhimu lakini unapaswa kuandamana na suluhisho.