Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Imeniwia vigumu kuzoea maisha ya soka England’ – Nunez

Darwin Nunez Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay na klabu ya Liverpool Darwin Nunez

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay na klabu ya Liverpool Darwin Nunez amesema tangia kusajiliwa Liverpool ameendelea kupata wakati mgumu kuzoea maisha ya soka ya nchini England.

Nunez aliyesajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili kutokea Benfica ya Ureno akizungumza hivi karibuni baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Rangers ameeleza kuwa ameendelea kuona mazingira ni magumu lakini atahakikisha anazoea na kufanya vizuri.

Takribani pauni milioni 64 zilitumika kumhamisha mchezaji huyo ambaye mpaka sasa amefunga goli moja tu kwenye Ligi Kuu England.

Moja ya mambo ambayo amesema yanampa shida England ni lugha ambapo Nunez mwenye umri wa miaka 23 anazungumza Kireno pekee wakati kocha Jurgen Klopp akizungumza kiingereza na Kijerumani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live