Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Imaisha hiyo! Mbappe kuvaa jezi ya Real Madrid msimu ujao

Kylian Mbappe To Madrid.jpeg Kylian Mbappe.

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaamu! Ndiyo, mshambuliaji wa Paris Saint German, Kylian Mbappe ameamua kwamba ataichezea Real Madrid msimu ujao baada ya kufikia makubaliano na kumaliza uvumi wa wapi atakwenda baada ya kuondoka Ufaransa.

Madrid imekuwa ikimfukuzia nyota huyo kwa muda mrefu na kwa mujibu wa mtandao wa The Sun, mwandishi wa Foot Mercto, Saint Aouna amesisitiza: "Mbappe atajiunga na Madrid."

Mbali na Madrid, Manchester United na Liverpool pia zimekuwa zikitajwa kuhusishwa na dili la nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa, huku mwenyewe akikataa ofa nono ya kutua kwenye moja ya timu za Ligi Kuu Saudi Arabia.

Na sasa, ile ndoto ya Madrid kumnasa nyota huyo inakwenda kutimia baada ya nyota huyo mshindi wa Kombe la Dunia 2018 kukaribia kuingia kwenye miezi sita ya mwisho ya mkataba wake PSG, jambo linalomwezesha kuanza mazungumzo na timu inayomtaka.

Mbappe 25, pia ana kipengele kwenye mkataba wake cha kuongeza mwaka mmoja kuendelea kuwepo Paris, lakini kwenye majira ya kiangazi mwaka jana aliandika barua kwa klabu hiyo akisema hana nia ya kufanya hivyo.

Mbappe aliingia kwenye mgogoro na timu hiyo kipindi cha maandalizi ya kuanza msimu huu wakati kikienda sambamba na dirisha la usajili na hivyo kuachwa kwenye safari, na inaelezwa PSG ilikubali ofa ya Al Hillal ya Saudi Arabia ya Pauni 259 milioni ili kumuuza, lakini mwenyewe alikataa dili hilo.

Mbappe alirudi kwenye kikosi cha PSG baada majadiliano ya kina na uongozi na pia kuachana na dili la Al Hilal, ambapo ameonyesha kiwango bora msimu huu na hadi sasa kaifungia timu hiyo mabao 18 na kuwa mchezaji muhimu kikosini.

Pia aliisaidia timu hiyo kutwaa Kombe la Ufaransa ikiichapa Toulouse kwa mabao 2-0, akifunga bao moja katika ushindi huo, huku lingine likifungwa na Lee Kang-in.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live