Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ilikuwa dabi ya hadhi ya fainali

Aucho Kibu Ilikuwa dabi ya hadhi ya fainali

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi bora yenye hadhi ya fainali kwani wachezaji wamepambana kuanzia mwanzo hadi mwisho hakika kila mmoja alikuwa anataka kupata ushindi.

Yanga SC katika zile dakika 15 za kipindi cha kwanza alikuwa anaweza kupata bao kwani Kennedy Musonda, Maxi Nzengeli, Jesus Moloko nyuma ya Clement Mzize walifanya high pressing katika safu ya ulinzi tya Simba SC na kuwalizimisha kufanya makosa mara kadhaa lakini hawakuweza kutumia nafasi hizo.

Bado kuna changamoto katika safu ya ushambiliaji ya Yanga, Mzize ni kama anakosa utulivu akifika lanogoni mwa mpinzani kwani zaidi ya nafasi za wazi ameshindwa kuzitumia ipasavyo.

Maxi yeye ni mzuri zaidi kwenye build - up anakuwa shapu pasi zake inakuwa sahihi ila ile touch zake zinakuwa sio sahihi. Gamond anapaswa atafute mtu sahihi atakaye simama pale mbele kama namba 9.

Khalid Aucho hakika ni bonge la holding, amefanya interceptions, kwneye 1vs1. Utamkimbua zile pasi zake, waow ametoa wakati mgumu kwa John Bocco kushindwa kufanya maamuzi sahihi.

Mudathir Yahya amekuwa katika kiwango bora amefanya build - up pamoja na recovering kwa wakati mmoja.

Huyu Yao Yao si wa kawaida, nilisema amekuja kuchukua namba yake moja kwa moja mwamba anajua kukaba na kushambulia anakasi na confedence.

Maxi huyu jamaa ni superb!!!!! Ubunifu, kasi na kujiamini pia onfedence akiwa na mpira mguuni ni vigumu kuchukua na leo katika wakati mgumu kwa mnyama.

What!! A defender pale kwa mkapa siku ya Simba Day watu walikuwa wanaimba Che Malone!!! Che Maloneā€¦ Che Malone leo kadhihirisha yeye ni mwamba kiasi gani anajua kunusa hatari, yupo vizuri kwenye kufanya buld - up, mipira ya juu haikuwa tatzo kwake anawahi kufika kwenye hatari hakika huu ni ukuta wa yeriko haswaa.

Ally Salim kwa mara nyengine anaibuka shujaa na kuifanya Simba kuwa bingwa wa ngao ya jamiii hakika kudaka penati 3 sio kazi rahisi, sasa ametukosoa wote tulikuwa tuna mzarau na kumuona ni kipa wa kawaida sana.

Nb: Hakika hii ilikuwa fainali bora na ya kuvutia wachezaji wamepambana kwa hali na mali ili kupata matokeo lakini ndoivo mwisho wa siku Simba ndio bingwa wa ngao ya jamiii 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: