Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ilanfya: Nilimsoma Diarra hatulii Golini

Ilanfya X Diarra Ilanfya: Nilimsoma Diarra hatulii Golini

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ihefu imeendeleza rekodi yake ya kuitesa Yanga baada ya juzi kuilaza mabao 2-1 huku straika wa timu hiyo, Charles Ilanfya akieleza namna alivyomsoma kipa Djigui Diara kabla ya kufunga bao la pili lililoipa ushindi.

“Mpira ni akili, licha ya kutangulia kutufunga hatukukata tamaa, tukafuata maelekezo na nilivyopata nafasi nikamsoma kipa hatulii alivyosimama nikaachia shuti hadi wavuni.

“Hakuna siri ya mafanikio zaidi ya kujituma, bado ni mapema na ligi ndio kama inaanza, kimsingi ni kuendelea kupambana kuhakikisha tunashinda kila mechi iliyo mbele yetu,” alisema Ilanfya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: