Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu yawapotezea makocha 100

Ihefu Ushindiiii Ihefu yawapotezea makocha 100

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Ihefu imesema licha ya kupokea maombi zaidi ya 100 ya makocha kutaka kufundisha timu hiyo, lakini hawana haraka yoyote isipokuwa wanaamini waliopo kwa sasa watafanya vizuri kutokana na kuijua vyema timu.

Timu hiyo haina kocha mkuu baada ya aliyekuwapo Moses Basena kutimuliwa hivi karibuni kutokana na matokeo yasiyoridhisha na kumuachia majukumu, Themi Felix.

Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Biko Scanda alisema tayari wamepokea maombi mengi ya makocha wa ndani na nje kutaka kazi kikosini humo, lakini kwa sasa hawajawa na mpango huo.

Alisema kwa kipindi hiki wameamua kuendelea kuwaamini waliopo kikosini chini ya Felix kutokana na vigezo vya kuwa kocha mkuu hivyo wanaendelea kusikilizia kwanza kujihakikishia mwenye ubora zaidi.

“Hatuna haraka kwenye suala la kocha, maombi ni zaidi ya 100, ila tumewaacha waliopo kwani vigezo wanavyo, lakini tunataka kocha anayewajua wachezaji wetu wazawa na tamaduni za timu yetu,” alisema.

Kigogo huyo aliongeza, wakati dirisha dogo linakaribia, wanasubiri mapendekezo ya benchi la ufundi, japokuwa kikosi walichonacho si kibaya isipokuwa ni kumpata kocha anayeweza kuwabadilisha.

“Tunaweza kuongeza, lakini timu yetu haina wachezaji wabaya, tunachohitaji ni kumpata kocha anayeweza kuwaandaa kifiziki na kuwabadilisha vitu vichache kwani uwezo wanao,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: