Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu yashusha Mnigeria

Taninu Benjamin Tanimu kutoka Nigeria

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ihefu yashusha beki mpya Benjamin Tanimu kutoka Nigeria, baada ya kubadilisha gia juu kwa juu.

Tanimu anakuwa Mnigeria wa pili kuingizwa katika kikosi hicho baada ya kiungo Morice Chukwu kusajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akianzia Singida.

Mchezaji huyo, msimu uliopita alijiunga na timu moja Hispania, kabla ya kurejea Nigeria katika klabu yake ya Bendel Insurance.

Beki huyo tayari amewasili kambini kule Arusha akiendelea na mazoezi na wachezaji wenzake na huenda akaonekana uwanjani wakati wowote kuanzia sasa.

Iko hivi. Awali ilikuwa aje mapema kujiunga na Singida Fountain Gate, lakini baadaye akahamishiwa Ihefu, akiwa ni miongoni mwa wachezaji wakigeni waliopelekwa katika kikosi hicho kipya.

Wachezaji waliohamishwa kutoa Singida kwenda Ihefu ni pamoja na Morice Chukwu, Marouf Tchakei, Joash Onyango, Mukrim Issa, Elvis Rupia,Khomeiny Khomeiny.

Ihefu imeshacheza mechi tatu za kirafiki mbili dhidi ya Mbuni na wameshinda zote, kisha kutoka sare mbili dhidi ya TMA na Polisi Tanzania.

Kwa sasa timu hiyo ipo jijini Arusha ikiweka kambi kabla ya kumalizia mechi ya kiporo cha duru la kwanza la Ligi Kuu Bara inayorejea leo kwa pambano la Kagera Sugar dhidi ya Yanga, kisha kuanza kujipanga kwa mechi za duru la pili la ligi hiyo inayoongozwa kwa sasa na Azam FC yenye pointi 31.

Chanzo: Mwanaspoti