Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu yashtuka mapema, hawataki presha

Ihefu Waifata Simba Kikosi cha Ihefu

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Ihefu kupoteza mchezo uliopita ikiwa nyumbani dhidi ya Simba kwa kulala kwa mabao 2-0 tayari benchi la ufundi limeshtuka kutokana na nafasi iliyokaa kwenye msimamo.

Mara ya mwisho Ihefu kupoteza uwanja wa nyumbani ilikuwa Novemba 11 ilipolala kwa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwa mabao ya Vitalisy Mayanga na Samwel Onditi aliyejifunga wakati bao la Ihefu likifungwa na Andrew Simchimba.

Ihefu sasa inashika nafasi ya saba kwa alama 33 huku wapinzani wake wa karibu ikiwa Kagera na Mtibwa Sugar ambao wamepishana alama chache.

Imesalia michezo minne ambayo inaweza kubadilisha upepo kwa kila timu kama itafanya vibaya kwenye michezo hiyo na kujikuta eneo la hatari zaidi.

Timu mbili kutoka Mbeya, Tanzania Prisons na Mbeya City zote zimekaa kwenye hali ya presha kutokana na mwenendo mbovu wao hasa mzunguko wa pili wa ligi.

Kocha msaidizi wa Ihefu, Zubery Katwila alisema wanafahamu wanachokifanya na wala hilo haliwapi presha japo wanatakiwa kuwa na tahadhari kubwa.

"Tumeliona hilo mapema ndio maana hata mchezo uliopita dhidi ya Simba nilisema namna matokeo yalivyotuathiri kwa kupoteza lakini ndio mchezo ulivyo.

"Tuna michezo iliyosalia nyumbani na ugenini hivyo kama tutafanikiwa kupata matokeo mazuri katika michezo mitatu basi itakuwa imetusaidia sana," alisema Katwila.

Ihefu kwa mara ya kwanza ilipanda Ligi Kuu msimu mwa mwaka 2020/21 kisha msimu uliopita ikashuka daraja na msimu huu ikarejea tena.

Chanzo: Mwanaspoti