Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu yaishitua Yanga

Ihefu Pic Data Ihefu yaishitua Yanga

Wed, 23 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Oliver AlbertMore by this Author Mbeya. Yanga inakamilisha mechi yake ya mwisho kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara leo kwa kuivaa Ihefu ugenini lakini kocha msaidizi wa kikosi hicho, Juma Mwambusi ameingiwa na hofu.

Mechi mbili mfululizo ambazo Ihefu imeshinda kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine Mbeya ndizo zimempa hofu Mwambusi, ambaye amekiri wanatakiwa kuikabili timu hiyo kwa tahadhari kubwa ili isiharibu rekodi yao.

Hadi sasa, Yanga ambayo ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 40 ndiyo timu pekee kwenye Ligi Kuu Bara ambayo haijapoteza mchezo wowote na inataka kupata ushindi leo ili imalize mzunguko wa kwanza kwa rekodi hiyo.

Yanga inatakiwa kuwa makini na Ihefu leo baada ya timu hiyo kuonyesha kiwango kikubwa katika mechi mbili zilizopita ilipoifunga Kagera Sugar mabao 2-1 kisha ikaichapa KMC bao 1-0.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz