Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu yaiba silaha za Yanga kimataifa

Ihefu Kimataifaaaa Ihefu yaiba silaha za Yanga kimataifa

Sun, 1 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Yanga jana ikishuka uwanjani kusaka tiketi ya kucheza makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh, benchi la ufundi na wachezaji wa Ihefu walikuwa bize kufuatilia mchezo huo ili kuisoma kwa lengo la kuja kuwabana vigogo hao watakapokutana nao kwenye mechi ya Ligi Kuu katikati ya wiki ijayo.

Yanga ilikuwa wenyeji wa Wasudani kwenye mechi iliyopigwa usiku wa jana katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na baada ya mechi hiyo itasafiri hadi jijini hapa kuwa wageni wa Ihefu mechi itakayopigwa Uwanja wa Higland Estate wilayani Mbarali, Jumatano ya Oktoba 4.

Timu hizo zinakutana kwenye uwanja huo huku zote zikiwa na kumbukumbu ya pambano lililochezwa Novemba mwaka jana na Yanga kupoteza kwa mabao 2-1 na kutibuliwa rekodi ya kucheza mechi nyingi mfululizo bila kupoteza ikikwamishwa ya 50.

Kocha Mkuu wa Ihefu, Zuberi Katwila alisema jana wapo kwenye maandalizi mazuri, na jana walipanga kuifuatilia Yanga, ilipokuwa ikicheza na Al Merrikh ili kupata mbinu za kuwabana.

Katwila alisema pamoja na mazoezi ya Kyela walipoweka kambi ya muda kupisha matengenezo ya uwanja wao kuwa mazuri, lakini lazima wawe makini kuendeleza ubabe kwa wapinzani hao nyumbani.

“Tunashukuru tumekuwa na maandalizi mazuri dhidi ya Yanga na tutatumia dakika 90 zao dhidi ya Al Merrikh kuwasoma madhaifu yao kujua wapi tuwabane, hatuwezi kucheza kwa historia isipokuwa mechi ni mechi na mbinu zinabadilika,”

“Vijana wanaonesha morali na kiu ya kuipambania timu, hatujawa na matokeo mazuri kwenye mechi tatu hivyo tunahitaji ushindi ili kujiweka pazuri na tunajua wapinzani wamekuwa na mwendelezo mzuri,” alisema Katwila aliyeiongoza timu hiyo katika mechi tatu ikishinda moja na kupoteza mbili ikishika nafasi ya 11.

Chanzo: Mwanaspoti