Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu yafuta uteja ikitoa dozi Mtibwa

Chirwa Obrey Lgt.jpeg Ihefu yapata ushindi mbele ya Mtibwa Sugar

Sat, 24 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Ihefu imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa kwenye Uwanja wa Highland Estate mkoani hapa.

Ushindi huo unaifanya timu hiyo kupanda nafasi ya 13 kwa pointi 17 na kuendelea kuwa na matumaini ya kukwepa rungu la kushuka daraja.

Pia matokeo hayo yanaifanya Ihefu kufuta uteja dhidi ya wapinzani hao kwani kabla ya mechi hiyo timu hizo zilikuwa zimekutana mara tatu na Mtibwa Sugar kushinda mbili na sare moja.

Mabao katika mchezo huo yamefungwa na Ismail Mhesa aliyeitanguliza Mtibwa Sugar kabla ya Joseph Mahundi aliyefunga mawili na Obrey Chirwa kuisawazishia Ihefu.

Huu ni ushindi wa kwanza wenye idadi kubwa ya mabao kwa Ihefu tangu ipande ligi kuu msimu huu na kulipa kisasi kwani raundi ya kwanza ililala 3-1.

Chirwa anafikisha mabao manne na asisti tatu baada ya mchezo wa leo, huku Mahundi akifikisha matatu msimu huu na kuendelea kuipa uhai Ihefu ambayo haikuwa na mwanzo mzuri.

Mtibwa Sugar inaruhusu kipigo hicho baada ya kucheza mechi tatu mfululizo bila kupoteza na kubaki nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kwa pointi 24.

Ihefu inashinda mchezo wake wa nne kwenye uwanja wa nyumbani na wa tano msimu huu huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 14 na kuruhusu 21.

Chanzo: Mwanaspoti