Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu wazidi kushusha nondo, sasa ni Mwantika

David Mwantika.jpeg David Mwantika amejiunga na Ihefu

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kumalizana na Straika Adam Adam, Ihefu imeendelea kujiimarisha kwa kumnasa beki wa kati, David Mwantika aliyewahi kutesa na timu kadhaa ikiwamo Azam FC.

Huo ni usajili wa pili kwa timu hiyo ya mkoani Mbeya katika kipindi hiki cha dirisha dogo baada ya kuwatema nyota wake watano.

Mwantika atakumbana na upinzani wa namba kikosini dhidi ya wenzake ikiwa ni Juma Nyosso, Leny Kissu,Said Juma Makapu na Ally Ally.

Ihefu bado haijawa na matokeo mazuri ikiwa nafasi ya 13 kwa pointi 20 na mchezo ujao itakuwa ugenini kukipiga na Yanga, mechi itakayopigwa Jumatatu ijayo.

Hata hivyo timu hiyo ya Wilayani Mbarali ndio yenye rekodi pekee kuisimamisha Yanga iliyokuwa imecheza mechi 49 bila kupoteza na sasa inaenda kuweka historia mpya ikisaka alama tatu muhimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live