Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu wapewa mchongo kuwamaliza Simba

Ihefu+pic Ihefu wapewa mchongo kuwamaliza Simba

Mon, 17 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Masoud MasasiIHEFU FC itaanza kusaka pointi kwa kuwakaribisha Simba kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku wakipewa ushauri wa kufanya usajili kwa umakini ili kikosi kiwe na ushindani mkubwa.

Ihefu ambayo maskani yake yapo Mbarali wamepanda daraja na watawakabiri mabingwa hao ambao wanatajwa kuwa ni miongoni mwa timu zenye kikosi bora.

Kocha Muhibu Kanu amewaambia Ihefu FC kuwa ili wawe bora ni lazima wafanye usajili wa maana ambao utakuwa na ushindani kwenye ligi itakayoanza Septemba 6 mwaka huu.

Kanu amezungumza hayo na Mwanaspoti Online leo Jumatatu Agosti 17, 2020 kuwa usajili mzuri ndio utawafanya Ihefu kufanya vizuri msimu ujao hivyo wanatakiwa kuwa makini kupata wachezaji wazuri.

“Ihefu wawe makini kwenye kusajili, wasajili wachezaji wazoefu na wale chipukizi ambao watafanya kikosi chao kiwe na mchanganyiko ambao utafanya wawe na timu bora.

“Nilicheza nao mechi mbili msimu uliopita wa Ligi Daraja la Kwanza nikiwa na Boma FC nimeona wana kikosi kizuri hivyo wanatakiwa kuongeza wachezaji wachache watakaowasaidia,” amesema Kanu na kuongeza

Chanzo: mwanaspoti.co.tz