Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu wameturahishia kazi ya kutwaa ubingwa - Ahmed Ally

Ihefu Wameturahishia Kazi Ya Kutwaa Ubingwa   Ahmed Ally.jpeg Ihefu wameturahishia kazi ya kutwaa ubingwa - Ahmed Ally

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Simba SC, Ahmed Ally amesema anawashukuru Ihefu FC kwa kuwafunga Yanga SC kwani wamewarahishia kazi na wao wanakwenda kuimaliza Jumapili katika dabi ya Kariakoo.

Ahmed ameyasema hayo leo Oktoba 30, 2023 kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo mkubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati.

"Ni mechi ambayo tunakwenda kuendeleza ubabe kwa watani zetu. Ili tujiridhishe kwamba msimu huu tutafanya vizuri ni kupata ushindi katika mchezo huo. Tunataka tuchukue ubingwa mapema sana, katika hili tunawashukuru Ihefu kwa kutusaidia kazi na sisi tunataka kuendeleza kuweka tofauti ya alama na Yanga SC."- Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live