Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu kuvunja rekodi kwa KMC leo?

Geita Nao Wataka Kuwachapa Yanga Kama Ihefu Ihefu FC

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyasi za Uwanja wa Uhuru leo zitawaka moto kwa kuzikutanisha KMC dhidi ya Ihefu mchezo utakaochezwa kuanzia saa 10:00 jioni.

Timu hizo zinakutana huku zote zikiwa zimetoka kushinda mechiĀ  za mwisho ambapo KMC iliichapa Geita Gold kwa mabao 2-1 huku Ihefu ikiifunga Yanga 2-1.

Wakati timu hizo zinakutana, rekodi zinaonyesha Ihefu haijawahi kupata matokeo mazuri nyumbani kwa KMC, hivyo mchezo huu ni wa rekodi kwa timu zote.

KMC imekutana na Ihefu mara nne huku kila mmoja ikiwa mbabe katika uwanja wake wa nyumbani na Ihefu katika mechi mbili za ugenini dhidi ya KMC zote imepoteza, huku KMC pia imepoteza dhidi ya Ihefu ikiwa ugenini.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Ihefu, Zuber Katwila amesema: "Kiufundi na kimaarifa tumejiandaa vizuri na tunajua tunakwenda kucheza na timu ngumu. Mchezo utaamuliwa kiufundi na kimbinu na tupo tayari kwa pointi tatu zingine."

Kwa upande wake, kocha mkuu wa KMC, Abdi Hamid Moalin amesema mchezo utakuwa mgumu na wanawaheshimu wapinzani wao, hivyo hawatataka kupoteza mbele yao kwani watacheza kwa tahadhari kubwa.

"Mchezo utakuwa mgumu na tunawaheshimu wapinzani wetu. Sisi kama timu malengo yetu ni kuhakikisha tunapata pointi tatu," amesema Moalin.

MECHI NNE ZILIZOPITA

Ihefu 1-0 KMC (19/12/2020)

Kmc 1-0 Ihefu (18/7/2021)

Kmc 2-1 Ihfeu (20/9/2022)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live