Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu SC haitaki kurudia makosa

Ihefu Ushindiiii Wachezaji wa Ihefu

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kusota kwa muda mrefu wakicheza mechi saba bila ushindi, hatimaye Ihefu juzi iliamka na kuilaza Tabora United mabao 2-1 huku benchi la ufundi likiwapa tahadhari mastaa wake kwa michezo inayofuata.

Ihefu ilicheza michezo saba mfululizo sawa na dakika 630 bila kupata ushindi tangu iliposhinda Oktoba 24 dhidi ya Yanga na kujikuta ikiwa nafasi tatu za mkiani na kuzuahofu kwa mashabiki.

Matokeo hayo yaliwafanya mabosi wa timu hiyo kumtimua aliyekuwa kocha wao, Moses Basena raia wa Uganda aliyeondoka bila kuonja pointi tatu akidumu kwa siku 50.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha msaidizi wa timu hiyo, Themi Felix alisema ushindi huo unafufua matumaini mapya katika kuanza kutembeza vipigo kwenye mechi zinazofuata.

Alisema walipitia kipindi kigumu licha ya kucheza vizuri lakini kwa sasa wanaanza upya kuhakikisha kila mchezo unaofuata wanapata ushindi ikiwamo Kombe la Azam Sports Federation (ASFC).

“Ni matokeo yanayorejesha morali na matumaini kikosini, lakini lazima tuanze kujipanga tena na mechi inayofuata ya ASFC dhidi ya Rospa FC.

“Tulipitia kipindi kigumu ila sasa tumejipanga na tunaanza upya kutimiza malengo yetu,” alisema Felix.

Kocha huyo aliongeza baada ya ushindi huo wachezaji wanapaswa kutobweteka kuhakikisha wanaendelea kupambana kusaka ushindi ili kujiweka nafasi nzuri.

Matokeo hayo yaliifanya Ihefu kukaa kwenye nafasi ya 13 ikiwa na pointi 13 na inatarajia kujitupa tena uwanjani kati ya Desemba 15 hadi 17 dhidi ya Rospa katika mchezo wa ASFC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: