Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu: Kesho ni fainali yetu na Yanga

Meximeee 087060362 Ihefu: Kesho ni fainali yetu na Yanga

Sat, 18 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Ihefu FC, Mecky Mexime ameeleza kuwa dhamira ya timu yake ni kucheza Michuano ya Kimataifa mwakani hivyo wanatakaka kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB.

Mexime leo amefunguka kuwa mchezo wao wa kesho Nusu Fainali ya kombe hilo dhidi ya Yanga SC ni fainali kwao hivyo Yanga wajipange kwani ameandaa shughuli nzito dimbani Sheikh Amri Abeid Arusha.

"Sisi fainali yetu itakuwa kesho, tutaingia kufa ua kupona. Tutaingia na mbinu zetu mimi na wachezaji wangu tutayatumia madhaifu yao kuwaadhibu na kujihadhari na ubora wao. Tunataka mashindano haya kwasababu na sisi tunataka kucheza Michuano ya Kimataifa," amesema Mexime.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live