Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu, Iponga zatakata Mbeya Pre Season

Mbeya Kumenoga Ihefu, Iponga zatakata Mbeya Pre Season

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Timu za Iponga (Malawi), Kyela DC, Rungwe na Ihefu zimeanza vyema michuano ya Mbeya Pre seasons baada ya kufanya kweli katika mechi zao za michuano hiyo.

Ligi hiyo ambayo ni msimu wa tatu, inafanyika kwenye uwanja wa Mwakangale wilayani Kyela mkoani hapa ambapo mwaka huu imekuwa na mabadiliko kufuatia kushirikisha timu kutoka nchi za Malawi na Zambia.

Jumla ya timu 16 zinashiriki ligi hiyo ambapo bingwa ataondoka na kitita cha Sh7 milioni, wa pili Sh5 milioni, wa tatu Sh3 milioni sambamba na medali kwa washindi hao.

Katika mechi za leo ilishuhudiwa Kalonga ikiambulia kisago cha mabao 3-2 dhidi ya Iponga zote kutoka nchini Malawi, huku Real Nakonde ikifa mabao 2-1 dhidi ya Kyela DC.

Mbeya Kwanza wanaojiandaa na championship msimu ujao nao walichezea kisago cha bao 1-0 dhidi ya Rungwe na Ihefu inayojiandaa na Ligi Kuu ikainyamazisha Tazara Rangers ya Zambia mabao 3-0 na kuwa timu pekee iliyoshinda kwa idadi kubwa ya mabao.

Ihefu ikiongozwa na makocha wake waliokuwapo msimu uliopita, John Simkoko na msaidizi wake Zuberi Katwila ilionesha soka safi, huku zikionekana sura mpya kwa wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.

Akifungua mashindano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ligi hiyo ni kuwapa fursa vijana kuonesha vipaji vyao na kuwaomba wadau kujitokeza kusapoti ili kufikia malengo.

"Lengo ni kuinua vipaji vya vijana na kutoa fursa kwao ukizingatia huu ni wakati wa usajili na tumeleta timu kutoka nje ya nchi ili kila mmoja aone pakutokea, lakini kama haitoshi tunaendeleza kile serikali inachofanya kupitia michezo " amesema Homera.

Kocha wa Mbeya Kwanza, Michael Mnyali 'Chuji' amesema anaamini kupitia michuano hiyo itasaidia kujiandaa na msimu ujao wa championship ikiwamo kupata wachezaji watakaoitumikia timu hiyo.

"Matokeo siyo kipaumbele sana, tunaangalia namna ya kusuka kikosi kwa ajili ya msimu ujao utakaoanza Septemba 2, naamini tutatoka na timu bora na tumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa uandaaji wa ligi hii na itatusaidia" amesema Chuji.

Chanzo: Mwanaspoti