Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ihefu FC kuweka kambi Mbeya

Mtibwa Sugar Zuberi Katwila Signs For Ihefu Fc 1bwhtnuvf7id61rxykq5oiz5ho Zuberi Katwila, Kocha wa Ihefu FC

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Ihefu FC Zuberi Katwila ameweka wazi kuwa kambi yao itakuwa Mbeya, kwa ajili ya kufanya maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23.

Ihefu imepanda ligi baada ya kupambana kwa msimu mmoja iliposhuka na kucheza Championship hivyo inarejea kwa mara nyingine tena.

Akizungumzia kambi hiyo, Katwila amesema kuwa, wanatarajia kukamilisha usajili hivi karibuni na kambi itakuwa Mbeya.

“Kambi yetu itaanzania hapa hapa Mbeya kwa muda wa wiki moja ambapo wachezaji tayari wameanza kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi.

“Usajili bado unaendelea ila tayari tumekamilisha hasa ukizingatia kwamba mapendekezo yetu na ripoti yetu inafanyiwa kazi na viongozi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live