Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ifike mahali Simba wamheshimu Matola - Jemedari

Jemedari Said The Voice Less Ifike mahali Simba wamheshimu Matola - Jemedari

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Kocha Roberto Oliviera kufurushwa Simba SC, mchambuzi wa masuala ya kabumbu, Jemedari Said, amesema Wekundu hao wa Msimbazi wanapaswa kumheshimu Selemani Matola maana amekuwa akiokoa jahazi mara kwa mara.

Jemedari ameandika hivi kupitia ukurasa wake wa Instagram;

Siku 2 baada ya kipigo cha AIBU kutoka kwa watani zao Yanga SC cha mabao 5-1 kwenye Ligi Kuu, uongozi wa Simba SC umemuondoa kocha wake mkuu Roberto Olveira kutoka Brazil. Zaidi ya Robertinho klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi Dar es Salaam imeachana na kocha wake wa viungo Corneille Hategimana.

Robertinho amekuwa kwenye shinikizo muda wote aliokuwa kwenye klabu hiyo bila kujali matokeo mazuri ambayo amekuwa akitapata kwenye Ligi.

Hatimaye Yanga wakaidhinisha talaka ya pande hizo mbili pale walipoizabua Simba mabao 5-1 na kuwatia aibu baada ya muda mrefu. Kwenye vilabu hivi hili lilitegemewa sana, haya yalikuwa ni matokeo ambayo lazima yangeomdoka na mtu au watu.

Nataka kuamini pia Simba hawajamaliza kuweweseka na kipigo, baada ya hapa wapo watakaofuata au yapo tutakayo sikia.

Kiungo na nahodha wa zamani wa timu hiyo Selemani Matola kama kawaida ameitwa kuokoa jahazi kama kocha msaidizi na kocha Mkuu atakuwa Dan Cadena ambaye ni kocha wa makipa.

Umefika wakati mashabiki wa Simba kumheshimu na kumthamini Selemani Matola amekuwa muokozi na kimbilio lao mara kwa mara kila wanapotimua makocha, lakini baada ya muda mfupi utasikia mashabiki wakimvunjia heshima gwiji huyu kwa kumpaka “Choo” kwa meneno ya kipuuzi puuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live