Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ifahamu Al Nassr maskani mapya atakayotua Ronaldo

B2ACC283 DE8C 4469 A190 BA55AF5AD13A.jpeg Cristiano Ronaldo

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Miongoni mwa habari ambazo zinasambaa sana kwenye tovuti mbalimbali za michezo duniani ni hatma ya staa wa zamani wa Manchester United, Cristiano Ronaldo ambaye anadaiwa kuhitajika sana na matajiri wa Saudi Arabia Al Nassr ambao wapo tayari kutoa zaidi ya Pauni 176 milioni kwa mwaka.

Kiasi hicho cha pesa ambacho atapewa kama mshahara ndicho kimezusha joto kwa wapenda soka wengi duniani kwani ataenda kuwa mchezaji wa kwanza kuvuna pesa nyingi zaidi duniani kiasi hicho kikiwa dili hilo litakamilika.

Je? Al Nassr ni timu ya aina gani, imewezaje kuwa na jeuri ya kuahidi kumlipa Ronaldo kiasi kikubwa kama hicho, mafanikio yao yapoje? twende sawa hapa.

HISTORIA YAO

Timu hii ilianzishwa Oktoba, 24, mwaka 1955 huko Riyadh, Saud Arabia na Zeid Bin Mutlaq Al-Ja’ba Al-Dewish Al-Mutair na ikaaanza rasmi kushiriki michuano mbalimbali kuanzia mwaka 1960 na miaka mitatu baadaye ikapanda hadi Ligi Kuu.

Kuanzia mwaka 1970 hadi 1980 ilishinda mataji manne ya Ligi Kuu, Kombe la Mfalme mara sita, matatu ya Crown Prince Cups na matatu ya Federation Cup.

Iliendelea kufanya vizuri hadi kufikia mwaka 2003 ambapo kuanzia hapo hadi 2007 ilipitia nyakati ngumu ikiwa pamoja na hatihati ya kushuka daraja.

Mpango ukasukwa upya na kutengenezwa timu ambayo ilianza kuonyesha matumaini mapya kuanzia mwaka 2014 hadi sasa.Mpango huo mpya ulikuwa ni pamoja na kuhakikisha timu inapata wadhamini na wafadhili wa kutosha wa kuwezesha kutoa pesa za kufanya usajili wa wachezaji bora wa kuisaidia timu.

Katika nyakati hizo ndipo zikajengwa akademi kwa ajili ya timu za vijana, wakati wote huu walikuwa wakitumia Uwanja wa Prince Faisal bin Fahd Stadium, lakini kuanzia mwaka 2020, walinunua uwanja wao uitwao Mrsool Park unaoweza kuingiza mashabiki wasiopungua 25,000.

KUMWAGA PESA WAMEZOEA

Achana na Ronaldo, lakini Al Nassr inaonekana kumwaga pesa ni tabia yao, kwa sababu katika orodha ya sajili tatu ghali zaidi kuwahi kufanywa nchini Saud Arabia wachezaji wao wawili wapo.

Usajili unaoongoza kwa sasa ni wa Matheus Pereira staa wa Brazil ambaye alisajiliwa na Al Hilal ambayo ndio mpinzani wa karibu wa Al Nassr, fundi huyu alisajiliwa kwa Euro 18 milioni.

Mastaa wengine wawili ni Mnigeria ambaye alisajiliwa na timu hiyo mwaka 2018 akitokea Leicester City kwa Euro 16 milioni. Vilevile Matheus Pereira naye ni staa mwingine ghali zaidi kwenye ligi hiyo ya Saudia na yeye alisajiliwa akitokea Atalanta ya Marekani kwa Euro 16 milioni.

Vilevile kwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi kwa sasa ikiwemo Vincent Aboubakar kutoka Cameroon hawalipwi mshahara mkubwa sana ingawa bado Al Nassr imeendelea kuweka rekodi ya kuwa timu anayotoka mmoja kati ya wachezaji wanaolipwa zaidi nchini humo ambaye ni Talisca anayepokea Pauni 5.3 milioni kwa mwaka.

Aboubakar ni staa wa pili kukunja pesa nyingi pale Al Nassr akiwa anavuta jumla ya 4.9 milioni kwa mwaka.

MAFANIKIO

Al Nassr imeshinda zaidi ya mataji 28 ya michuano mbalimbali ya ndani na nje ya Saudia, mataji kati ya hayo ni yale ya Ligi Kuu ambapo mara ya mwisho kulichukua ilikuwa msimu wa 2018-19, sita ni ya Kombe la Mfalme, matatu ya Kombe la Mwana wa Mfalme.

Kwenye upande wa kimataifa, Al Nassr imechukua taji moja la Asian Cup Winners’ Cup mwaka 1997-98, haijawahi kuchukua kombe la Ligi ya mabingwa zaidi ilifika fainali mara moja tu mwaka 1995.

CANNAVARO ALIPITA

Beki pekee kuwahi kuchukua Tuzo ya Ballo D’or, Fabio Cannavaro aliwahi kuifundisha timu hii kwa miezi sita.

Cannavaro alianza kuifundisha timu hiyo Oktoba 2015 hadi February 2016 ambapo alichana nayo na kutimkia zake China.

Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Italia akiwa na timu hiyo aliiongoza Al Nassr kwenye mechi 13 na akashinda mechi tano tu huku tano zikiisha kwa sare na tatu wakafungwa.

Chanzo: Mwanaspoti