Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idris Mbombo ampagawisha Kocha Azam FC

Idris Mbombo Amkosha Mshambuliaji wa Azam FC, Idris Mbombo amekuwa na kiwango bora

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC, Kally Ongala amesifu uwezo unaoendelea kuonyeshwa na staa wake, Idris Mbombo huku akiweka wazi amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi chake msimu huu.

Kauli ya Ongala inajiri baada ya Mbombo kufunga mabao mawili na kufikisha matano msimu huu wakati kikosi hicho kilipoibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Akizungumza Kally alisema haukuwa mchezo mwepesi kutokana na jinsi ambavyo wapinzani wao walivyorejea kipindi cha pili ingawa ubora wa mastaa wake ndio unaompa jeuri.

“Mbombo ni mchezaji mzuri sana na naamini akiendelea hivi atafika mbali, kwangu nafurahia kuona wachezaji wakijitoa kwa ajili ya timu yao kwani ndio msingi uliopo,” alisema Kally. Kally aliongeza kadiri wanavyozidi kushinda ndivyo ambavyo wanavyojiweka karibu na kutimiza malengo yao.

“Ni mapema sana kuzungumzia suala la ubingwa lakini sisi kama benchi la ufundi kazi yetu ni kuhakikisha kila mchezo wetu tunapata matokeo mazuri kisha mengine yatafuata mbeleni.”

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alitoa pongezi kwa wachezaji wote na benchi la ufundi kutokana na matokeo mazuri wanayoendelea kuyapata katika Ligi Kuu. Ushindi huo kwa Azam ni wa nne mfululizo msimu huu ikiwa ni kwa mara ya kwanza baada ya awali kushinda (1-0) dhidi ya Simba Oktoba 27, Ihefu 1-0 Oktoba 31, kisha 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji Novemba 9.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live