Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Iddrisu, Ahamada wachomolewa Azam FC

Aloi Ahmada Vs Kakolanya Mlinda mlango wa Azam FC, Ali Ahmada

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Makipa wawili wa Azam FC, Abdulai Iddrisu na Ali Ahamada wameondolewa kwenye usajili wa kikosi hicho baada ya kuonekana watakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha mbalimbali waliyoyapata mwaka jana.

Iddrisu anauguza jeraha la bega lake la mkono wa kushoto alilofanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini sambamba na Ahamada anayesumbuliwa na goti la mguu wa kushoto huku akiondoka na kwenda Ufaransa kwa ajili ya uchunguzi wa matibabu zaidi.

Makipa hao wote ambao wamekuwa ni chaguo la kwanza watakaa nje ya uwanja kwa takribani miezi minne hadi mitano hivyo viongozi kushtuka na kuwaondoa kwenye usajili ili kupisha nyota wengine wapya waliosajiliwa dirisha hii kuongeza nguvu.

Mastaa wapya waliosajiliwa na kikosi hicho ni kipa, Mohamed Mustafa aliyetokea Al-Merrikh ya Sudan, beki wa kati, Yeison Fuentes aliyetoka timu ya Leones FC na mshambuliaji, Franklin Navarro aliyesajiliwa kutoka Cortulua FC ya kwao Colombia.

Mbali na kuondolewa mastaa hao, timu hiyo ilitangaza kuachana na aliyekuwa mshambuliaji, Idris Mbombo aliyetua Nkana ya Zambia.

Chanzo: Mwanaspoti