Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Iddi Nado aipa ushindi Azam mbele ya Singida FC dakika za jioni

Azam Vs Art Solar 7 Azam wakishangilia.

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam imeendeleza wimbi la ushindi kwenye Ligi Kuu Bara baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Big Stars, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Azam ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Cheikh Sidibe dakika ya 10 huku Marouf Tchakei wa Singida akichomoa dakika ya 57 kisha Idd Seleman 'Nado' akaipatia bao la ushindi mwishoni mwa mchezo dakika ya 90.

Matokeo haya yanaifanya Azam kushinda michezo yote mitatu ya Ligi Kuu Bara msimu huu ikianza na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tabora United, (3-1) na Tanzania Prisons kisha kushinda leo 2-1 na Singida Big Stars.

Kwa upande wa Singida hiki ni kipigo cha kwanza kwao msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kuanza michezo miwili kwa suluhu ikianza dhidi ya Tanzania Prisons na Tabora United ambayo yote ilichezwa Uwanja wa Liti.

Tangu Singida imepanda Ligi Kuu Bara msimu uliopita haijawahi kuifunga Azam kwenye Uwanja wa Azam Complex kwani mara ya mwisho zilipokutana ilipoteza bao 1-0 Oktoba 3, mwaka jana lililofungwa na Sospeter Bajana.

Matokeo haya yanaifanya Azam kushika nafasi ya tatu na pointi zake tisa baada ya kushinda michezo yake yote mitatu ya mwanzo wa Ligi Kuu Bara huku kwa upande wa Singida ikisalia nafasi ya 12 baada ya kukusanya pointi mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: