Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Iddi Nado: Ndoto yangu imetimia kucheza Klabu Bingwa

Iddy Nado Complex Iddi Nado.

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Klabu ya Azam, Iddi Nado ameeleza furaha yake baada ya kuingia kwenye michuano ya Klabu bingwa barani Afrika.

Nado amesema hayo leo wakati Kikosi cha Azam FC kikiondoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar kwa ajili ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB ambayo itapigwa Jumapili, Juni 2, 2024 dhidi ya Yanga SC.

"Mechi ilikuwa ngumu na ilikuwa inaamua tunakwenda kumaliza katika nafasi gani, lakini tunamshukuru Mungu tulipata alama tatu. Nina furaha sana kwa sababu hii ndiyo mara yangu ya kwanza kucheza michuano ya klabu bingwa Afrika, ndoto yangu ilikuwa kushiriki michuano hiyo.

"Azam msimu huu hatuna kombe kwa hiyo kombe hilo linaweza likawa kombe letu," amesema Nado.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live