Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibwe: Simba wanatokaje Chamazi?

Azam X Ibweee Hasheem Ibwe na wachezaji wa Azam FC.

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Azam, Hasheem Ibwe amesema kuwa nafasi yao ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao watajihakikishia kesho endapo wataifunga Azam FC.

Ahmed amesema hayo kuelekea mchezo huo wa Ligi utakaopigwa kesho katika Dimba la Azam Complex Chamazi huku Azam akiwa nafasi ya pili alama 57 na michezo 25 na Simba nafasi ya 3 akiwa na alama 50 na michezo 24.

“Tunakwenda kucheza na timu ambayo haina furaha yoyote licha ya ushindi ambao wamekuwa wakiupata.

“Kwenye Kombe la Muungano hatusemi tulilidharau lile Kombe lakini nyakati ziliamua kuwa wao wapate lile Kombe. Mungu nae aliamua hawa wapate mana furaha imetoka upande wao.

“Mchezo wa NBC ni mchezo tofauti, kuna Kipre Junior, una Gibril Sillah, kuna James Akaminko, Feisal Salum, Abdul Suleiman ‘Sopu’ lakini nina GAFA Yousuph Dabo pamoja na kocha Bruno Ferry wanatokea wapiii?” amesema Ibwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live