Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibrahimovic: Ligue 1 bado inanihitaji

Zlatan Ibrahimovich Milan Zlatan Ibrahimovi?

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa PSG na sasa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic anaamini kuwa soka la Ufaransa linaporomoka bila yeye kuwepo huku akisema kuwa hata uwepo wa Kylian Mbappe, Lionel Messi na Neymar hautoshi.

Ibrahimovic alifurahia muda mwingi akiwa na miamba hao wa Ufaransa Paris Saint-Germain kati ya 2012 na 2016, na alifanikiwa kushinda mataji 12 ya nyumbani yakiwemo mataji manne mfululizo ya Ligue 1.

Mshambuliaji huyo wa raia wa Sweden alifunga mabao 156 akiwa na PSG kwa upande wake, amezidiwa na Edinson Cavani ambaye ana mabao 200, na Mbappe ambae mpaka sasa ana mabao 188 katika historia ya klabu hiyo, ingawa kurejea kwake kwa mabao 0.87 kwa kila mechi ni bora zaidi ya wachezaji hao wote wawili.

Vile vile Ibrahimovic anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha Milan mwaka 2023 baada ya kupata jeraha la goti (anterior cruciate ligament) mwishoni mwa msimu uliopita huku akidai kuwa Ligue 1 inateseka kwa kukosekana kwake.

Akiongea na Canal+, Ibrahimovic alisema: “Tangu nilipoondoka Ufaransa, kila kitu kinaanguka, hakuna tena somo lolote la kuvutia Ufaransa inanihitaji, lakini sihitaji Ufaransa.

Aliongezea kwa kusema kwa hata kama una Mbappe, Neymar, na Messi bado haitoshi, wakati wachezaji hapo ndio wanaiwakilisha ligi hiyo kwasasa kutokana na ubora ambao wanao mpaka sasa huku Kylian akiwa na mabao 11, Neymar 10 na Messi 7 wakiwa wamefunga jumla ya maba0 28.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live