Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibenge amtaka Dube, awapelekea Azam milioni 764 zao

Ibenge Dube Prince Dube.

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hii ni baada ya kutokea vuta ni kuvute kati ya mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube na klabu yake ya Azam FC.

Sasa klabu ya Al Hilal ya Sudan inayofundishwa na kocha Florent Ibengé imegonga hodi katika klabu ya Azam FC na kutoa ofa ya Dola 200,000 (Tsh Milioni 509) ili kumnasa mshambuliaji huyo.

Hata hivyo ofa hiyo imekataliwa na Azam FC ambao wamesema dau la kumchukua mchezaji huyo ni Dola 300,000 (Tsh Milioni 764) kama mkataba wake unavyosema Mkataba wa Prince Dube na Azam FC amebakisha mkataba wa miaka miwili na nusu Azam FC utakaomuweka kwenye timu hiyo mpaka mwaka 2026.

Taarifa za ndani kutoka chanzo chetu cha kuaminika upande wa Prince Dube kimethibitisha kuwa Dube kwa sasa hafikirii kurejea Azam FC na hata kujiunga na klabu nyingine yoyote ila tu lengo kuu kuachana na klabu hiyo na kuwa mchezaji huru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live