Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibenge amrudisha Mukoko Congo

Kaze Pic Mukoko Data Ibenge amrudisha Mukoko Congo

Sun, 28 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Khatimu NahekaMore by this Author Kiungo mkabaji wa Yanga Mukoko Tonombe ameitwa katika kikosi cha Taifa lake cha DR Congo kinachojiandaa na michezo miwili ya kuwania kucheza Fainali za Mataifa Afrika.

Mukoko ameitwa katika orodha ya wachezaji 44 ambao watachujwa na kupatikana 23 watakaounda kikosi kitakachocheza mechi mbili dhidi ya Gabon na baadaye Gambia.

Awali Mukoko aliwahi kuichezea timu hiyo akiwa na kikosi chake cha zamani cha AS Vita lakini atue Yanga hakuwahi kuitwa mpaka sasa kocha wake wa zamani Florent Ibenge amemrudisha tena.

Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa pili kuitwa katika timu hiyo akitanguliwa na aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo ambaye hata hivyo hakufanikiwa kupenya na kuingia katika orodha ya mwisho.

Mtihani mkubwa kwa Mukoko ni kupenya katika orodha ya mwisho ya wachezaji 23 ambapo rekodi inaonyesha asilimia kubwa nafasi kubwa hupenya wachezaji wanaocheza nje ya Taifa hilo hasa kutoka Ulaya.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz