Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibenge aingia mchecheto mbele ya Simba

Ibenge Florent Kocha Ibenge

Wed, 23 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya kuzitazama rekodi zake anapocheza na Simba, Kocha Mkuu wa RS Berkane, Florent Ibenge, amekiri kukutana na upinzani mkali dhidi ya timu hiyo katika michuano ya kimataifa.

Ibenge amekutana na Simba mara nne katika michuano ya kimataifa wakati alipokuwa akiinoa AS Vita ya DR Congo ambapo katika michezo hiyo amepoteza mitatu na akishinda mmoja.

Ibenge kwa sasa akiwa kocha mkuu wa RS Berkane ya nchini Morocco, anatarajiwa kukutana na Simba katika mchezo wa Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Februari 27, nchini humo, ambapo timu hiyo imetoka kupoteza katika mchezo uliopita kwa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live