Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibenge adokeza jambo Simba

Ibenge Florent Azungumza Ibenge adokeza jambo Simba

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

uzoefu iliyonayo Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, kiwango cha mastaa wake kwa sasa, vimemfanya kocha mkubwa Afrika Florent Ibenge kusema Simba msimu huu inatoboa kimataifa.

Simba inatarajiwa kuvaana na Horoya ya Guinea, mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa Klabu Afrika utakaopigwa Februari 11 na kocha huyo amesema anaamini Simba watapata ushindi mzuri kwenye mchezo huo.

Kocha huyo wa Al Hilal ya Sudan, aliichambua Simba kuanzia namna inavyocheza, mastaa iliyonayo na uzoefu wake wa kucheza michuano ya CAF akaipa asilimia kubwa ya kupata ushindi dhidi ya Horoya, Jumapili.

Ibenge ambaye ambaye timu yake imecheza michezo mitatu ya kirafiki hapa nchini alisema licha ya kutoka nayo sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kirafiki na Simba, lakini timu hiyo ya Msimbazi ina mastaa wenye uwezo mkubwa na wanaotumia akili zitakazowasaidia kwenye michuano ya CAF.

"Simba kwenye michuano ya CAF ina uwezo mkubwa, binafsi naipa nafasi ya kufanya vizuri kwenye mchezo wao wa kwanza licha ya kucheza ugenini, ina wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kusoma mbinu na wakabadili matokeo.

"Michuano ya CAF inahitaji akili kubwa, mbinu, matumizi ya nafasi kwa hilo Simba imefanikiwa ndiyo maana imekuwa na mfululizo wa kufanya vizuri miaka ya hivi karibuni bado naamini wanaweza kufanya mambo makubwa tena msimu huu, wachezaji wanajua nini wafanye na kwa wakati gani wakiwa uwanjani, mara nyingi timu inatakiwa kuwa na mastaa wa hivi kama unataka kupata ushindi," alisema Ibenge ambaye timu yake inacheza soka la kasi na kulinda kwa wakati, akiwa na historia ya kushika nafasi yab pili kwenye Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika akiwa Vita Club.

Ibenge ni kocha anayelijua vizuri soka la Afrika, mwaka jana akiwa na RSB Berkane ya Morocco, timu hiyo ilicheza dhidi ya Simba, ilishinda mabao 2-0 nyumbani, ilipigwa bao 1-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini aliiongoza kuchukua Kombe la Shirikisho.

"Ukiachana na mechi za ugenini, Simba ni hatari zaidi ikicheza kwenye uwanja wake, ina mashabiki ambao wana nguvu ya kuisapoti timu yao, wachezaji morali zao zinakuwa juu zaidi kuhakikisha wanawapa raha mashabiki wao, nimekuwa hapa ukiacha mchezo ambao nimecheza nao lakini pia nimeangalia mechi zao kadhaa za ligi, ni timu bora," alisema.

Wakati kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliviera anatambulishwa aliahidi kuifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali kwenye michuano hiyo ni kama anaendana na mawazo ya kocha Ibenge.

Mbali na kucheza na Simba, Al Hilal ilikuwa hapa nchini kwa zaidi ya wiki moja, ambapo ilicheza pia mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam na kushinda 1-0, ikacheza na Namungo na kutoka sare.

Simba inaratajia kuondoka kesho Jumatano mchana kwenda Guinea kuifuata Horoya, hiyo ni kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa timu hiyo na wanakwenda na mastaa wao wote wakubwa.

IMESHINDA MECHI HIZI CAF

Big Bullets 0-2 Simba (Sept 10/2022)

Simba 2-0 Big Bullets(Sept 14/2022)

Primeiro de Agosto 1-3 Simba (Oktoba 9/2022)

Simba 1-0 Primeiro de Agosto (Oktoba 16/2022)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live