Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibenge: Tumekuja kutafuta ushindi

Ibenge Pic Data Ibenge: Tumekuja kutafuta ushindi

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KESHO Jumapili kuanzia saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kutapigwa mechi kali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba ya Tanzania na AS Vita Club ya Congo DRC.

Mchezo huo ni wa marudiano katika hatua ya Makundi ambapo utazikutanisha timu hizo mbili kutoka kundi A baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Congo, Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Baada ya kuwasili Tanzania usiku wa kuamkia leo, kocha mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge amesema kuwa wamekuja kutafuta matokeo ambayo yatafufua matumaini yao ya kusonga mbele hatua inayofuata.

"Tumekuja kucheza, ni mechi ngumu ambayo tutahitaji matokeo chanya ili kujiweka mahali salama kuelekea hatua inayofuata. Nadhani dakika 90 za mchezo huo zitakuwa nzuri na zenye ushindani mkubwa," amesema Ibenge.

Katika mchezo huo Simba mwenye alama 10 kileleni mwa kundi A juu ya Al Ahly wenye alama saba, atahitaji matokeo ya sare au ushindi ili kufuzu hatua inayofuata ya robo fainali huku AS Vita aliye nafasi ya tatu na alama nne atahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele.

Mchezo wa mwisho hatua ya makundi Simba itacheza na Al Ahly ugenini huku AS Vita watawakaribisha Al Merrikh nyumbani.

Related Msuva apumzishwa Dar



Aussems, Migne waiteta Simba


Atapigwa mtu nyingi
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz