Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibenge: Mayele mfungaji bora

Mayele 123 Ibenge: Mayele mfungaji bora

Fri, 8 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA wa zamani wa Fiston Mayele, Florent Ikwange Ibenge, amesema kuwa mshambuliaji huyo wa Yanga atatwaa kiatu cha ufungaji bora msimu huu kutokana na ubora wake.

Kocha huyu alimfundisha Mayele wakati yupo As Vita ya nchini Congo. Ibenge ameyasema hayo baada ya juzi Mayele kufunga bao la kideoni walipoichapa Azam 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa sasa ndiye kinara wa mabao ligi kuu akiwa amefunga 11, akifuatiwa na Reliants Lusajo mwenye mabao 10. Akizungumza na Championi Ijumaa, Ibenge amesema Mayele ni mchezaji mwenye kiu ya kiatu cha ufungaji bora.

“Mayele ni mchezaji mzuri sana na mimi kila nikipata muda wa kuongea naye huwa namshauri aendelee kupambana, atafikia malengo yake aliyojipangia msimu huu.

“Kwa kiwango alichonacho na anachokionyesha kwa sasa, anaweza kuchukua kiatu cha ufungaji bora maana ni mpambanaji sana na unaona kabisa ana nia ya kukipata na mimi namuombea akipate.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live