Kocha Mkuu wa Al Hilal, Florent Ibenge amesema mashabiki wa Al Ahly ndio walikuwa mwiba kwao na kusababisha kushindwa kucheza mechi hiyo kama walivyokuwa wamepanga.
Ibenge amesema hayo baada ya mechi ya raundi ya mwisho ya Makundi ya Kombe la Mabingwa Afrika kati ya Al Hilal dhidi ya Al Ahly SC kumalizika nchini Misri huku Hilal ikiambulia kichapo cha bao 3-0 na kuondoshwa kwenye michuano hiyo.
"Mashabiki wa Al Ahly walikuwa ni sababu kubwa ya hofu kwa wachezaji wangu, hatukuweza kuhimili mechi na kucheza kwenye mfumo wetu kama tulivyopanga usiku wa leo," amesema Ibenge.
Timu zilizofanikiwa kutinga robo fainali CAFCL.
Walioongoza kwenye makundi yao;
Raja CA
Mamelodi Sundowns
Espérance de Tunis
Wydad AC
Nafasi ya pili kwenye makundi;
Al Ahly
JS Kabylie
CR Belouizdad
Simba SC.