Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibenge Aichambua Simba, Awataja Sakho, Morrison

Ibenge Florent Ibenge Aichambua Simba, Awataja Sakho, Morrison

Thu, 24 Feb 2022 Chanzo: Ibenge Aichambua Simba, Awataja Sakho, Morrison

KOCHA Mkuu wa RS Berkane ya nchini Morocco, Florent Ibengé, amekichambua kikosi cha Simba huku akiwataja baadhi ya wachezaji wazoefu na tishio watakaoibeba timu hiyo.

RS Berkane wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Simba katika mchezo wa tatu wa Kombe la Shirikisho Afrika Kundi D utakaochezwa Februari 27, mwaka huu kwenye Uwanja wa Municipal de Berkane nchini Morocco.

Kocha Ibenge alisema Simba ina faida ya kuwa na wachezaji wengi ambao wamecheza kwa pamoja kwa muda mrefu na wazoefu wa michuano ya kimataifa, huku pia kukiwa na wachezaji ambao wana uwezo mkubwa wa kuamua mechi kama Bernard Morrison na Pape Sakho.

“Simba si ngeni kwangu, nimekutana nayo mara kadhaa katika michuano ya kimataifa, nimekitazama kikosi chao cha sasa na kuna wachezaji wengi ambao nimekutana nao miaka mitatu iliyopita na mpaka leo wapo na wanafanya vizuri.

“Ni msaada mkubwa sana kwa Simba na wanaisaidia timu, ukiachana na hao, pia ina wachezaji wanye uwezo mkubwa wa kuamua matokeo, Morrison namfahamu ni mchezaji mzuri, mchezo uliopita alifanya hivyo, lakini Sakho pia ni mchezaji mzuri.

“Kuhusu wachezaji ninaowakumbuka kuna kipa Manula (Aishi) na Mkude (Jonas) ambaye ni kiungo, ni wachezaji wazuri na wa siku nyingi ndani ya Simba,” alisema kocha huyo. Simba itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa michezo mitatu kati ya minne waliyocheza dhidi ya Kocha Ibenge kipindi akiwa anainoa AS Vita ya DR Congo.

Chanzo: Ibenge Aichambua Simba, Awataja Sakho, Morrison