Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ian Maatsen anahesabu dakika Aston Villa

Ertret Ian Maatsen anahesabu dakika Aston Villa

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Inaelezwa Ian Maatsen amefauli vipimo vya afya na anaweza kusaini mkataba wa miaka sita kuitumikia Aston Villa ndani ya siku hizi mbili.

Inaelezwa Villa italipa Pauni 37.5 milioni kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa fundi huyu wa Chelsea aliyecheza kwa mkopo Borussia Dortmund msimu uliopita. Mkataba wake unamalizika mwaka 2026.

GALATASARAY imefikia hatua nzuri katika mazungumzo ya kumsajili beki wa Man United, Aaron Wan-Bissaka katika dirisha hili.

Bissaka anadaiwa kutaka kuondoka Man United kwa kile kinachoelezwa kwamba kocha Erik ten Hag hana mpango naye kwa msimu ujao.

Mabosi wa Gala, wamekuwa wakimtumia staa wao Wilfried Zaha amshawishi Bissaka kwani waliwahi kucheza wote Crystal Palace.

KWA mujibu wa tovuti ya Daily Mail, David Beckham ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa Inter Miami yupo katika mazungumzo na wawakilishi wa beki wa zamani wa Manchester United, Raphael Varane kwa ajili ya kuipata saini yake katika dirisha hili.

Miami ambayo ina mastaa kibao kama Lionel Messi, Luis Suarez na Sergio Busquets, inamtaka Varane kwa ajili ya kuboresha eneo la ulinzi.

BENFICA imeziambia timu zinazohitaji huduma ya kiungo wao Joao Neves kwamba zitatakiwa kutoa Pauni 100 milioni ili kuipata saini yake.

PSG ni kati ya timu zinazotamani kumsajili staa huyu lakini haitaki kulipa kiasi hicho pesa badala yake inataka kutoa Pauni 63 milioni. Mkataba wake unamalizika mwaka 2028. Msimu uliopita alicheza mechi 58 za michuano yote na kufunga mabao sita.

MANCHESTER United imetuma ofa ya Pauni 46 milioni kwenda Everton kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo Amadou Onana, ambaye pia anawindwa na Arsenal.

Gazeti la Mundo Deportivo linaeleza kwamba, Onana alikuwa katika rada za Barcelona pia ambayo rasmi imeondolewa katika mchakato huo kwa sababu haitoweza kulipa pesa inayofikia dau hilo.

STRAIKA wa Stuttgart na Guinea, Serhou Guirassy anatarajiwa kufanya uamuzi wa wapi atacheza msimu ujao ndani ya siku chache zijazo wakati vigogo mbalimbali barani Ulaya ikiwa pamoja na Arsenal, Borussia Dortmund na Chelsea zote zikionekana kutaka kumsajili. Mkataba wake una kipengele cha kuuvunja kwa Pauni 15 milioni tu.

ARSENAL inadaiwa kufikia makubaliano na Sporting Lisbon kwa ajili ya kumnunua straika wao raia wa Sweden, Viktor Gyokeres katika dirisha lijalo. Kwa mujibu wa gazeti la Leonino, Arsenal italipa Pauni 75 milioni kwa ajili ya kukamilisha dili hilo. Mkataba wake una kuna kipengele cha kuuvunja kwa Pauni 86 milioni lakini Lisbon wanaishusha.

Chanzo: Mwanaspoti