Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndo Star Boy Saka

Bukayo Saka Bukayo Saka

Tue, 28 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bukayo Saka ni moja kati ya mawinga bora kwa sasa Ulaya kutokana na kile anachokifanya uwanjani, tunaweza kusema ndiye staa wa Arsenal.

Arsenal imekuwa katika ubora mkubwa msimu huu hasa ndani ya Premier League, wakiwa kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya Manchester City wanaoshika nafasi ya pili.

Saka mwenye miaka 21, yupo katika ubora akiwa anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza msimu huu ndani ya Premier League kufunga mabao 10 na asisti 10.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Crystal Palace, Saka alifanya mambo makubwa, kocha wake, Mikel Arteta alifunguka kwamba: “Nafikiri timu yangu imefanya vizuri na wengine wamefanya vizuri hasa kwa juhudi binafsi.

“Ila kwa ujumla wachezaji wangu wamekuwa bora wakipambana, wengine wamezidi kuimarika na kuwa bora zaidi, ubora huu unatakiwa kuendelea kuonekana hata katika michezo mingine.”

Saka ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Star Boy, ameendelea kutisha na kuonyesha ubora wake ndani ya Arsenal kama rekodi na takwimu zake kwa namba namna zinavyozungumza hapa.

Ni kati ya wachezaji nane wa Arsenal waliofanikiwa kufunga na kuasisti zaidi ya mabao 10 ndani ya Premier League. Wachezaji wengine wa Arsenal waliowahi kufanya hivyo ni Thierry Henry, Dennis Bergkamp na Cesc Fabregas.

AMEKUWA na mchango wa mabao 22 ndani ya Premier League akifunga 10 na asisti 12, ni moja kati ya rekodi bora katika ligi tano bora Ulaya.

AKIWA na miaka 21, Saka amekuwa mchezaji mdogo zaidi kuweka rekodi hiyo ya mabao na asisti, awali aliishikilia Febregas akiwa na miaka 22, akifunga na kuasisti zaidi ya mabao 10.

Saka amehusika katika mabao ya Arsenal kwa asilimia 33.3 katika ligi. ERLING Haaland na Harry Kane ni wachezaji pekee ndani ya Premier wamekuwa na mchango zaidi ya Saka japo hao wawili ni mastraika, lakini yeye ni winga.

WINGA huyo amefanya takolini za uhakika mara 46 kuliko mchezaji mwingine ndani ya ligi, akiwa na asilimia 37.

KATIKA mabao yake 12 manne yamemfanya kuwa mchezaji bora wa mchezo na matano alifunga dhidi ya big six.

SAKA ana jumla ya mashuti aliyozalisha 124 ndani ya Premier League msimu huu, ni wachezaji wanne pekee ndiyo wamemzidi.

WINGA huyo kiwango chake uwanjani ni 3.2xG, kwa Arsenal anazidiwa na Gabriel Martinelli pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: