Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndo Pilato wa Fainali ya Kombe la Dunia Argentina vs Ufaransa

ISzymon Marciniak.jpeg Huyu ndo Pilato wa Fainali ya Kombe la Dunia Argentina vs Ufaransa

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka la Kimataifa, Fifa, limethibitisha kwamba, Szymon Marciniak atakuwa mwamuzi wa fainali ya Kombe la Dunia Jumapili kati ya Argentina na Ufaransa.

Marciniak tayari amesimamia michezo ya miamba hiyo miwili iliyofika fainali nchini Qatar.

Alichezesha kwenye ushindi wa 2-1 wa Ufaransa katika hatua ya makundi dhidi ya Denmark na ushindi wa 16 bora wa Argentina dhidi ya Australia.

Mwamuzi huyo ambaye pia alichezesha mechi za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, ameonesha kadi tano pekee za njano katika mechi zake mbili za michuano ya mwaka huu na bado hajatoa kadi nyekundu.

Baadhi ya waamuzi wamekosolewa kwa uchezaji wao katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia, akiwemo Antonio Mateu Lahoz, aliyetoa kadi 15 za njano katika ushindi wa robo fainali ya Argentina dhidi ya Uholanzi.

Shirikisho la Soka la Morocco limewasilisha malalamiko kwa Fifa kuhusu uchezaji wa Cesar Ramos kama mwamuzi wakati wakifungwa kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa, Jumatano.

FIFA pia ilitangaza  kuwa mwamuzi wa Qatar, Abdulrahman Al Jassim atachezesha mchezo wa kuwania nafasi ya tatu Jumamosi kati ya Croatia na Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live