Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndo Eng. Hersi, Mhuni kutoka Kinondoni Moscow

Eng. Hersi Said Sd Huyu ndo Eng. Hersi, Mhuni kutoka Kinondoni Moscow

Fri, 1 Mar 2024 Chanzo: Farhan Kihamu

THE UNITED REPUBLIC OF WAHUNI, pichani ndio Rais wao kwenye hiyo nchi ya Wahuni! Kichwa cha habari kinasema Mhuni kutoka Kinondoni Moscow aliyeishi ndoto zake, passport ndani ya nchi ya Wahuni ni Mission wanataka kuiteka Afrika, Mhuni ameipeleka Yanga fainali ya Shirikisho, Mhuni ameipa ubingwa back to back Yanga na bado anaendelea.

Baada ya mafanikio ya kihistoria msimu wa 2022/23 Kocha Nabi alibisha hodi ya kutaka kuondoka, akamwambia nimekusikia na nakutakia kila la heri, likaja benchi zima mpaka wakina Kaze akawaambia nimewasikia nawatakia kila la heri, Mhuni akaendelea kuvuta tai yake vizuri kusubiri nani mwingine anataka kuondoka, kumbuka tayari amempoteza Feisal Salum hapo.

Wakati anaendelea na mipango yake ofisini akapokea simu ya Yannick Bangala anataka kuondoka akamjibu Fresh Asante MVP, akapokea simu ya Djuma Shabaan kuwa anaondoka akawambia njoo ofisini upitie barua yako, mwisho ni pigo la kubwa Top Scorer Fiston Mayele, akamwambia Fresh kwa heri ya kuonana Predator, asanteni nyote kwa kumbukumbu na page ikaandika THANK YOU za kutosha.

Mhuni akarudi tena kwenye ramani ya vita, akaweka alama maeneo yote ambapo watu wameondoka na kuyatambua kama No Man’s Land kisha kusuka upya mapambano! Yanga imeanza msimu bila MVP, bila bench karibia lote la Ufundi, bila Top Scorer, bila Winger hatari BM33, bila Yannick, bila Feisal wala Djuma Soldat ya Bemba, bado haikuwa na tatizo! Mhuni karuhusu watu halafu kaenda kuvunja rekodi ya klabu.

Msela na Mhuni on a Mission! Anatemba na Presidential Emergency Satchel, muda wowote mahali popote, linalipuka. Mwandishi nae ni MHUNI tu anatokea nchi hii, si alisema Yanga wana wakati mgumu?

Chanzo: Farhan Kihamu