Charles William M'Mombwa ni kijana aliyezaliwa Machi 14, 1998, katika eneo linaloitwa Baraka nchini Congo DR.
Yeye na familia yake walikimbilia Tanzania, ambako walikaa kwa zaidi ya muongo mmoja, kisha wakaishi katika Casula, Kusini-Magharibi mwa Sydney.
Baadaye wazazi wake walihamia nchini Australia akacheza mpira kama baba yake, akafanikiwa kusajiliwa kama kiungo wa klabu ya A-League Macarthur FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
M'Mombwa nafasi yake uwanjani ni Midfielder-attacking Midfield na Baba mzazi wa M'Mombwa alikuwa mchezaji wa kandanda na kocha alipokuwa akiishi DR Congo.
M'Mombwa alijiunga na timu ya vijana ya Mt Druitt Town Rangers mwaka 2017, kisha akapelekwa CCM Academy ya nchini Australia ambayo aliitumikia mpaka mwaka 2019 kisha kujiunga na timu ya wakubwa ya Central Coast Mariners.
Baada ya kupitia akademi ya Mariners, M'Mombwa aliichezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza katika mechi ya Kombe la FFA dhidi ya Adelaide United August mosi mwaka 2018.
Mnamo tarehe 20 Novemba 2020, Macarthur FC ilitangaza kuinasa saini ya M'Mombwa kwa msimu wao wa kwanza,nakufanikiwa kufunga goli lake la kwanza Juni 12 mwaka 2020,katika muda wa ziada kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Central Coast Mariners,ukiwa ni mfululizo wa Fainali za 2020-21 A-League.
Kwa sasa anachezea timu ya Macarthur FC inayoshiriki ligi kuu ya nchini Australia na amechagua kulitumikia taifa la Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Charles M’mombwa (25) ndiye aliyefunga goli la Taifa Stars katika Mchezo wa kwanza wa Kuwania kufuzu Kombe la Dunia nchini Marekani.
Alicheza mechi yake ya kwanza na pekee ya Ligi ya A-League kwa Central Coast nakupoteza nyumbani magoli 8-2 dhidi ya Wellington Phoenix FC.