Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndo Aziz Ki wa ASEC

Dfb Aziz Kiii Huyu ndo Aziz Ki wa ASEC

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa yanga, Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso, amekuwa na wakati mzuri msimu huu 2023-2024 akiuanza kwa kasi ya hatari akiwa ni miongoni mwa nyota wetu wanaotupa kiburi.

Aziz Ki msimu huu hadi sasa amefanikiwa kucheza mechi saba za kimashindano ambazo ni dhidi ya Azam (Ngao ya Jamii), Simba (Ngao ya Jamii), ASAS Djibouti (Ligi ya Mabingwa Afrika), KMC (Ligi Kuu), ASAS Djibouti (Ligi ya Mabingwa Afrika), JKT Tanzania (Ligi Kuu) na Al Merrikh (Ligi ya Mabingwa Afrika).

Kiungo huyo katika mechi hizo 7, amehusika kwenye magoli 6, akifunga mabao 4 na kutoa assists 2.

Mechi ambazo Aziz Ki amefunga ni dhidi ya Azam (1), ASAS Djibouti (1), KMC (1), JKT Tanzania (1). Huku akitoa asisti dhidi ya Al Merrikh (1) na JKT Tanzania (1).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: